Staa wa Bongo Fleva Harmonize (kulia) na Dj D Ommy (kushoto) wa Clouds wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuchukua tuzo.
Tuzo za AFRIMMA ambazo hutolewa kila mwaka kwa Waafrika mbalimbali waliofanya vizuri kwenye sekta mbalimbali hasa za burudani, zimetolewa Dallas, Texas nchini Marekani.
Wasanii wa Tanzania walioshinda tuzo ni Staa wa Bongo Fleva nchini, Diamond Platnumz, Harmonize na Dj D Ommy wa Clouds FM ambaye ameshinda Tuzo ya Dj Bora wa Afrika kupitia shoo mbalimbali ikiwemo XXL na AMPLIFAYA. Harmonize ameshinda tuzo ya msanii bora chipukizi Afrika 2016 huku Diamond Platnumz akishinda ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki.
Staa wa Bongo Fleva nchini, Harmonize (kushoto) akiwa na staa wa muziki wa Nigeria, Tekno.
Wengine waliochukua tuzo ni Wakenya, Sauti Sol walioshinda kundi bora la muziki Afrika ikiwa ni tuzo iliyokua ikiwaniwa na Radio na Weasel wa Uganda, Os Moikanos wa Angola, Bracket wa Nigeria, Mi Casa South Africa, R2bees wa Ghana, Bana C4 wa Congo DRC na Yamoto Band wa Tanzania.
Mkenya Akothee ameshinda msanii bora wa kike Afrika Mashariki, tuzo iliyokua inawaniwa na Victoria Kimani wa Kenya, Vanessa Mdee na Linah wa Tanzania, Aster Aweke na Tsedenia wa Ethiopia, Knowles wa Rwanda na Sheebah Karungi wa Uganda.
Mkenya mwingine ni staa wa Gospel Kenya Willy Paul ambaye ameshinda tuzo ya Best Gospel Act iliyokua ikiwaniwa na Frank, Uche, Sinach wa Nigeria, SP Koffi na Sonnie wa Ghana, Icha wa Congo na Ntokozo wa South Africa.
FULL LIST WINNERS AFRIMMA 2016:
Best New Comer Afrika – Harmonize
Best Male East – Diamond Platnumz
Best Dj Afrika – Dj D Ommy
Best Male West Africa – Olamide (Nigeria)
Best Female West Africa – Efya
Best Male North Africa – Amr Diab
Best Female North Africa – Ibtissam
Best African DJ USA – Dj Dee Money
Best Male Central Africa – C4 Pedro
AFRIMMA Video of the year – Brother brother Bisa Kdei
Best Female Central Africa – Daphne
Music Producer of the year – Masterkraft
Best male South Africa – AKA
Sautisol, Akothee na brothers wengine Dallas Texas
Best African Dancer – Mshindi Brenda Derry ( Cameroon) tuzo hii iliwaniwa pia na Mtanzania Dancer wa Diamond Platnumz aitwae Mose Iyobo.
Best Female Southern Africa – Chikune
Best Rap Act – Phyno (Nigeria)
Best African Group – Sauti Sol (Kenya)
0 comments:
Post a Comment