www.kenethngamoga.blogspot.com

Awasilisha ombi la kubadili jinsia yake arabuni

Mwanamke mmoja amekuwa mtu wa kwanza katika Umoja wa Falme za kiarabu kuwasilisha ombi la kutaka kubadilishwa jinsia chini ya sheria mpya inayohalalisha upasuaji wa kufanyia mabadiliko sehemu za siri

Kumekuwa na mjadala kama huo katika jeshi la Marekani
Image captionKumekuwa na mjadala kama huo katika jeshi la Marekani
Mwanamke mmoja amekuwa mtu wa kwanza katika Umoja wa Falme za kiarabu kuwasilisha ombi la kutaka kubadilishwa jinsia chini ya sheria mpya inayohalalisha upasuaji wa kufanyia mabadiliko sehemu za siri .
Wakili wa mwanamke huyo Ali al-Mansouri ameambia vyombo vya habari nchini humo kwamba siku zote mteja wake amehisi kuwa yeye ni mwanamume, na amekuwa akipokea matibabu ya kimwili na kiakili kwa miaka minne iliyopita.
Ameeleza kuwa hisia za mteja wake ni kwamba mwili wake haudhihirisha jinsia yake ya kweli na ni jambo lililomsababishia wasiwasi na mawazo mengi.
Mansouri ameeleza kuwa tume ya matibabu ilipendekeza kwamba afanyiwe upasuaji huo.
Sheria hiyo mpya ya afya ya Umoja wa falme za kiarabu ilioidhinishwa mapema mwezi Septemba, inaruhusu upasuaji huo kwa misingi ya matibabu.
"upasuaji huo... Unaruhusiwa iwapo ni sehemu ya matibabu kwa matatizo ya kijinsia , kama itakavyoshauriwa na tume ya matibabu itakayoundwa kwa lengo hilo," sheria hiyo inasema.
Mahakama ya Abu Dhabi itasikiliza kesi hiyo tarehe 28 mwezi Septemba.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment