Baada ya usiku wa June 30 2016 kushuhudia robo fainali ya kwanza ya Euro 2016 na kushuhudia timu ya taifa ya Ureno inayoongozwa na mchezaji bora wa dunia mara tatuCristiano Ronaldo wakitinga robo fainali, usiku wa July 1 2016 ilikuwa zamu ya Waleskutinga katika hatua hiyo.
Wales wamefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali kwa akuifunga timu ya Ubelgijikwa jumla ya goli 3-1, magoi ambayo yalianza kufungwa dakika ya 31 na Ashley Williams ikiwa zimepita dakika 18 toka Ubelgiji wapate goli la kuongoza kupitia kwaRadja Nainggolan, magoli ya mawili ya mwisho ya Wales yalifungw na Hal Robson Kanu dakika ya 55 na Sam Vokes dakika ya 85.
Kwa matokeo hayo timu ya taifa ya Wales sasa ni rasmi itakutana na timu ya taifa yaUreno katika mchezo wa nusu fainali, hiyo itakuwa ni nusu fainali inayowakutanisha wachezaji ghali wa dunia Gareth Bale na Cristiano Ronaldo lakini ni mastaa ambao wanacheza klabu ya Real Madrid
.
0 comments:
Post a Comment