www.kenethngamoga.blogspot.com

Vijijini wahitaji elimu kutambua simu bandia

Wito huo umetolewa mkoani Mtwara na mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, wakati wa ufunguzi wa warsha kwa wanafunzi wa sekondari na wadau wengine wa huduma zinazodhibitiwa, iliyoandaliwa na Jukwaa la watumiaji Tanzania (TCF)
Wito huo umetolewa mkoani Mtwara na mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, wakati wa ufunguzi wa warsha kwa wanafunzi wa sekondari na wadau wengine wa huduma zinazodhibitiwa, iliyoandaliwa na Jukwaa la watumiaji Tanzania (TCF), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki za mtumiaji itakayofanyika kitaifa Machi 15 mwaka huu mkoani Mtwara.
Amesema kutokana na maeneo mengi ya vijijini kuwa na miundombinu migumu kwa kuweza kufikiwa na vyombo vya habari ambavyo vinatumika kutoa elimu hiyo, wananchi wengi wanakosa kupata elimu na itawafanya waendelee kutumia na kununua simu hizo ambazo ni bandia.
Kwa upande wake, katibu mtendaji wa baraza la ushauri kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mhandisi Goodluck Mmari, amesema maadhimisho hayo mwaka huu yanafanyika mkoani Mtwara kwa kuzingatia sababu mbalimbali ikiwamo kuwapo kwa fursa nyingi za kiuchumi zinazotokana na uwepo wa rasilimali za Mafuta na Gesi asilia.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment