www.kenethngamoga.blogspot.com

Mabadiliko yaiongezea pato Hospitali ya Muhimbili

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Hospital ya Taifa ya Muhimbili Prof.Laurence Muselu katika mahojiano maalum na East Africa Radio na kuainisha kuwa mikakati waliyojiwekea imeanza kuzaa matunda ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuwasaidia 
Watumishi wakiwa nje ya Jengo la Mwaisela lililopo ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Hospital ya Taifa ya Muhimbili Prof.Laurence Muselu katika mahojiano maalum na East Africa Radio na kuainisha kuwa mikakati waliyojiwekea imeanza kuzaa matunda ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuwasaidia watanzania wote bila kuwabagua.
Prof.Muselu amesema kuwa uongozi wa Hospital hiyo umeyafanyia kazi malalamiko mbalimbali yaliyokua yanatolewa na wagonjwa waliofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbaliza kimatibabu.
Aidha Mkururgenzi huyo amesema kuwa wamehakikisha kuwa morali ya watumishi imepanda kutokana kuhakikisha kila mfanyakazi anafanyakazi kwa kutimiza malengo waliokubaliana sambamba na kuwalipa malimbikizo yao mbalimbali waliyokuwa wanadai kwa kipindi cha nyuma.
Aidha Prof. Maselu ameongeza kuwa mpaka sasa hawajajua pato la wastani wanalopata hospitalini hapo lakini kwa kipindi cha kujiangalizia miezi sita ya kwanza watatoa tathmini ya kipato kinacho ingia Hospitalini hapo
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment