Headlines za uhamisho wa Neymar mwaka 2013 kutoka Santos kujiunga na FC Barcelona zinazidi kuchukua headlines kila kukicha, leo November 23 2016 suala hilo limechukua headlines mpya baada ya muendesha mashitaka kuomba Neymar na Rais wa zamani wa FC Barcelona Sandro Rosell wahukumiwe.
Muendesha mashitaka amemuomba jaji Jose Perals kumuhukumu Neymar miaka miwili na kumuhukumu Rais wa zamani wa FC Barcelona Sandro Rosell miaka mitano jela kwa kosa la rushwa na ukwepaji kodi katika uhamisho wa Neymar 2013.
Hata hivyo klabu ya FC Barcelona itapigwa faini ya pound milioni 7.2 kwa kosa hilo pia, kama utakuwa unakumbuka vizuri Sandrol Rosell alijiuzulu nafasi yake ya urais wa FC Barcelona mwaka 2014 kufuatia tuhuma za uhamisho wa Neymar ambazo zimegubikwa na ujanja ujanja.
0 comments:
Post a Comment