www.kenethngamoga.blogspot.com

Samatta azidi kutikisa nyavu Ulaya

Mshambuliaji wa Tanzania Mbwana Ally Samatta nyota yake imezidi kung'ara baada ya kuifungia klabu yake ya KRC Genk bao dhidi ya Club ya KV Oostende katika ligi kuu ya Belgium Pro League.
Samatta alifunga goli hilo dakika ya 24 ambapo ni mara yake ya kwanza kuingizwa katika kikosi cha kwanza (first eleven) katika timu hiyo.
Samatta alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu katika mechi hiyo dakika ya 24 akifuatiwa na Balley dakika ya 39, Pozuelo dakika ya 81 na Camargo dakika ya 88 wakati Club ya Kv Oostende ilijipatia goli moja kupitia kwa Siani dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo timu ya KRC Genk iliibuka kidedea kwa bao 4-1 ambapo bao la Samatta ni bao lake ya pili tangu ajiunge na Club hiyo.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment