www.kenethngamoga.blogspot.com

RICHI MAVOKO ATUA KWA DIAMONDPLATNUMZ

Mwanzo zilikuwepo tetesi kuwa Msanii Rich Mavoko ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake 'Naimani' kuwa amesaini mkataba wa kusimamiwa kazi zake chini ya Label ya WCB ambayo ipo chini ya msanii Diamond Platnum.
Tetesi hizi ziliendelea kubaki tetesi hadi jana ambapo imewekwa wazi kuwa ni kweli msanii huyo hivi sasa yupo chini ya WBC.
Kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio msanii Harmonize alithibitisha kuwa ni kweli Rich Mavoko kwa sasa yupo chini ya label hiyo ambayo mpaka sasa ina wasanii kadhaa akiwepo yeye mwenyewe Harmonize, Raymond aliyekuwa Tip Top Connection pamoja na Rich Mavoko.
"Unajua mwanzo zilikuwa ni tetesi lakini naweza kusema 'its official' sasa Rich Mavoko yupo chini ya WCB, hivyo kusema kuwa Rich Mavoko amenyoosha mikono kwa Diamond si vizuri kwani watu wanaweza kupata picha tofauti maana si unajua watu wanaweza kupokea jambo kwa maana na ikaleta picha mbaya wakati ni jambo la kawaida" alisema Harmonize
Lakini mbali na hilo msanii huyo amedai kuwa mwezi wa tatu anatarajia kuachia albam yake ya kwanza na kusema ameamua kuachia albam hiyo kwa lengo la kujitengenezea CV katika muziki.
"Tumekaa na uongozi wangu mwezi wa tatu nitaachia albam yangu ya kwanza hivyo kwenye label yangu nitakuwa msanii wa kwanza kutoa albam lakini nafanya hivi ili kupata heshima maana bila kuwa na albam huwezi kumwambia msanii mkubwa wewe ni msanii mkubwa Afrika Mashariki wakati huna albam hata moja, hivyo natoa albam yangu nipate heshima na si kwa ajili ya mapato" alisema Harmonize
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment