www.kenethngamoga.blogspot.com

Ifahamu Ijumaa Kuu kiundani.

Siku kama ya leo saa tisa alasiri, ni maarufu kama Ijumaa Kuu, katika nyumba za ibada za Kikristo, kimya hutanda, mishumaa huzimwa na kuashiria kuwa ni siku ya majonzi. Ijumaa Kuu ni siku ambayo Wakristo duniani kote hukumbuka mateso aliyoyapata Yesu
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeipa thamani siku hii kwa kuitangaza kuwa ya mapunziko. Siku hii huadhimishwa kwa ibada inayoambatana na kusoma mistari ya Biblia inayoelezea undani wa matukio yaliyosababisha kusulubiwa kwa Yesu Kristo miaka zaidi ya 2000 iliyopita.
Hii ni siku ambayo inatajwa kuwa na maana kubwa katika imani ya Kikristo. Waumini wanaamini kwamba, kusulubiwa na kufa kwa Yesu, kumeleta ukombozi duniani kote.
Ijumaa Kuu haithibitishwi tu na vitabu vya dini, bali hata machapisho ya kihistoria, yanathibitisha juu ya kusulubiwa na kufa kwa Yesu. Huadhimishwa kwa ibada huku zikitawaliwa na mistari na nyimbo za maombolezo ya kufa kwa Yesu.
Rangi za vitambaa vipambwavyo kanisani, huwa ni zile zinazoashiria maombolezo. Hufanyika tangu asubuhi na inapofika saa tisa, muda unaosadikiwa kuwa ndipo Yesu alikata roho, makanisa hutawaliwa na kimya kiambatanacho na kuzima mishumaa ndani ya kanisa.
Katika muda huo wengi hutafakari namna walivyokombolewa kwa damu ya Yesu. Makanisa mengi, vikundi mbalimbali kama vile watoto, vijana na wanawake, hutumia siku hiyo kuonesha maigizo ya kusulubiwa na kufa kwake.
Aidha Kipindi hiki watu wengi wamejiwekea utaratibu wa kufunga kila Ijumaa wakati wengine hufunga siku 40 kabla ya Pasaka. Suala la kufunga linaloambatana na kutenda yaliyo mema, halina muda wala kikomo.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment