“Game ya nyumbani najua itakuwa ngumu kwasababu Chad ni wazuri wanawachezaji professionals wanacheza kwa kujiamini na wakija kucheza hapa watacheza kwa kujiachia kwahiyo mechi itakuwa ngumu”, anasema Mkwasa ambaye uso wake unaonesha kufurahishwa na matokeo ya ushindi wa ugenini licha ya kusisitiza mchezo ulikuwa mgumu kutokana na hali ya hewa na ubora wa wapinzani wake.
“Wao wanaimani wanaweza wakapata ushindi kama walivyowahikupata ushindi katika kipindi kilichopita, lakini na sisi tumejipanga kuhakikisha historia haijirudii, kama walitufunga mara ya kwanza kwetu sisi tumeamua kupata ushindi mwingine tukiwa nyumbani.
“Nawaomba watanzania waje kwa wingi ku-support wachezaji na wawe pamoja na wachezaji watuombee kwa Mungu”.
“Timu imerejea ikiwa na majeruhi wawili ambao ni Mwinyi Kazimoto na Kelvin Yondani ambaye alipata matatizo baada ya mechi lakini wote wanaendelea vizuri, ndiyo kwanza tumerudi daktari wa timu ataangalia na atatupa taarifa kamili itakuwaje”.
Stars itacheza mchezo wa marudiano dhidi ya Chad March 28 siku ya Jumatatu ya Pasaka kwenye uwanja wa taifa, Dar es Salaam.
Dondoka hapa chini umsikilize mwenyewe Mkwasa anavyofunguka kuhusu mchezo wamarudiano dhidi ya Chad utakaopigwa taifa
0 comments:
Post a Comment