www.kenethngamoga.blogspot.com

Wastara atoa ujumbe mzito kwa wanaume

Msanii wa filamu hapa nchini wastara juma jioni ya desemba 10 ametoa ujumbe wenye maneno mazito kwa wanaume kwa kuwataka kuwaheshimu sana wanawake na kubainisha baadhi ya sababu za kuwaheshimu
kupitia akaunti yake ya instagram wastara ameshare na mashabiki wake .......
# MWANAMKE ● Anabadili Jina lake ● Anahama nyumbani kwao ● Anaacha familia yake ● Anaondoka na wewe ● Anajenga nyumba na wewe ● Anabeba ujauzito wako ● Ujauzito wako unabadili umbo lake ● Anakua mnene ● Anateseka chumba cha uzazi kwa maumivu makali kwa ajili ya mtoto wako. ● Na mtoto akizaliwa anasubiri umpe jina unalolipenda. Mpaka kifo chake atakufanyia kila kitu, kukupikia, Kusafisha nyumba yako, Kuwatunza wazazi wako, Kulea watoto, Kubana matumizi, Kukushauri, Kuhakikisha unapumzika, Kujenga mahusiano mazuri ya familia, Wakati mwingine anaweza hatarisha afya yake, Uhai wake kwa ajili yako. Anakufumania analia kisha anakusamehe. Mwanaume Muheshimu Mwanamke Katika Maisha yako, Sababu kuwa Mwanamke si jambo rahisi. Mfanye Mwanamke kuwa kiumbe mwenye furaha pindi unapokua nae maana Muda wa furaha kwake ni mdogo sana. Heshima kwa Wanawake wote Duniani.
A photo posted by Wastara Sajuki (@wastara84) on
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment