Mwaka 2015 ni mwaka uliotangazwa na wasanii wengi wa Bongo Fleva kutoa album zao,lakini mpaka mwezi wa 11 mwaka huu hakuna msanii ambaye kafanikiwa kuachia album licha ya baadhi ya wasanii kusema kuwa watamuuzia Said Fela lakini pia hazijafanikiwa kutoka ikumbukwe mpango huu umesimama zaidi ya miaka 3 wasanii kuachia album.
Inawezekana Navykenzo wakaufungua mwaka 2016 rasmi kwa kuachia album yao ambayo wamesema itakua na utofauti wa vitu vingi ikiwemo mfumo wa uuzwaji wa album hiyo>>’Mpaka sasa hivi album imeshakamilika na inaitwa Above in minutes,ndani yake kuna wasanii wa nje na wa ndani kama Young Dee na G Nako ina ngoma 8,tutauza Online na kwenye Cd lakini itakua ni kwa Oda tu hata kama ni online itakua ni oda tu ukishalipia siku ikitoka unapewa ya kwako baada ya hapo itakua ni ngumu kuuza‘
0 comments:
Post a Comment