Mahakama ya Wilaya ya
Kilombero imemuhukumu kifungo cha nje
cha miezi sita aliye kuwa Diwani wa Kata ya Ifakara ambae ni mgombea Ubunge kwa Tiketi ya Chadema Bwana Peter Lijualikali baada ya kupatikana na kosa la kutumia
lugha ya matusi na kutishia kuua kwa maneno.
Hukumu hiyo imetolewa
Mahakamani hapo na Hakimu Bigilwa Nyakato
ambapo ameeleza kuwa Lijualikali ametenda makosa hayo mnamo Novemba 26
mwaka 2014 dhidi ya aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Ifakara Akrey Muhenga.
Hakimu Nyakato amesema kuwa
ametoa adhabu hiyo kwa mujibu wa sheria na kuwa Mtuhumiwa ndio kosa lake la
kwanza kufikishwa Mahakamani na kumpa onyo akajifunze upya kuishi na jamii na
asipatikane na kosa lolote la jinai akifanya hivyo ndani ya miezi hiyo adhabu
kali atapewa zaidi ya hiyo.
Hata hivyo Hukumu hiyo imetolewa bila ya mtuhumiwa kufikishwa Mahakamani hapo
kutokana na hukumu hiyo mgombea huyo wa nafasi ya ubunge kwa tiketi ya chadema katika jimbo la kilombero anaendelea na kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu mwezi oktoba
.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na
Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata
habari mpya.
0 comments:
Post a Comment