www.kenethngamoga.blogspot.com

KINGUNGE amejiondoa rasmi CCM!! kayasema haya..,,

Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombare Mwiru leo ametangaza kujiondoa ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM na sasa atakuwa mwananchi huru.
Kingunge amezungumza leo mbele ya waandishi wa Habari akiwa nyumbani kwake Kijitonyama, Dar es salaam.
Amesema kutokana na matukio yaliyotokea katika kumpata mgombea Urais kupitia chama chake ni tofauti na ilivyokuwa mwaka 1995 na 2005 hivyo ameamua kuondoka ndani ya chama hicho na sasa yupo huru.
Kingune amesema hawezi kuhimili chama kisichojiendesha bila katiba na anajua uamuzi wake utawasumbua baadhi ya ndugu zake, wazee na makada wengine.
Mwanasiasa huyo amesema kwa sasa hakusudii kujiunga na chama kingine chochote kwa kuwa amekuwa mwanaharakati kwa miaka 61.
Pia amesema yeye ni raia na ana haki zake za kisiasa na kijamii na ataendelea kuwa na mahusiano mazuri na nchi yake..”Hali ya sasa jinsi ninavyoona vijana, wafanyakazi, wakulima wanataka mabadiliko na mimi nipo upande wa mabadiliko kwa sababu wakati tukiwa TANU tulifanya mabadiliko na kuunda CCM”KINGUNGE
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment