Wana mashabiki wengi, miongoni mwao tayari ni mamilionea (wa shilingi), wapo wenye mijengo, magari ya kifahari, miradi ya biashara, makampuni, endorsements na vitu vingine. Hawa ndio wasanii 12 wa Tanzania wenye nguvu zaidi mwaka 2014.
Diamond Platnumz
Diamond Platnumz ndiye msanii anayeandikwa zaidi kwenye vyombo vya habari Afrika Mashariki kwa sasa. Hadi sasa Diamond amefikia hatua ambayo haijawahi kufikiwa na msanii yeyote wa Tanzania. Ndiye msanii mwenye show nyingi zaidi kwa sasa.
Kimataifa 2014 umekuwa wa mafanikio zaidi kwake kuanzia kutajwa kuwania vipengele viwili kwenye tuzo za MTV MAMA, BET Awards, kushiriki kwenye wimbo uliokutanisha mastaa takriban 20 wa kampeni ya ‘Do Agric’ ‘Cocoa na Chocolate, pamoja na wimbo ‘Africa Rising’ uliomkutanisha na wasanii kama Mi Casa Music, Davido, Sarkodie na Tiwa Savage.
Pia pamoja na kufanya wimbo na Davido, Diamond ameshafanya collabo na wasanii wengine wa Nigeria wakiwemo Iyanya, Waje na Dr Sid pia hivi karibuni ameshirikishwa na kundi la Afrika Kusini, Mafikizolo.
Pamoja na kukosa tuzo za kimataifa alizotajwa kuwania, staa huyo mwaka huu alivunja rekodi kwa kuchukua tuzo zote saba alizotajwa kwenye KTMA na pia kushinda tuzo za watu zilizotolewa June 27.
Akiwa na video mbili mpya kibindoni, moja ya wimbo aliofanya na Iyanya na ile ya wimbo wake ‘Mdogo Mdogo’, Diamond ana uhakika wa kuendelea kuutawala mwaka 2014.
Lady Jaydee
Judith Mbibo aka Lady Jaydee ndiye msanii wa kwanza wa Tanzania kufikisha likes 300,000 kwenye mtandao wa Facebook huku sasa idadi ikiwa ni zaidi ya 329,000. Tangia June mwaka jana alipofanya show yake ya miaka 13 ya muziki wake na kuijaza Nyumba Lounge watu wasipate pa kukanyaga, Lady Jaydee haoneshi dalili za kusimama. Baada tu ya kutoka kwenye Coke Studio Africa, Jaydee alishiriki kwenye wimbo maalum kwaajili ya kombe la dunia wa Coca Cola, ‘The World is Ours’. Pamoja na show zisizo katika, biashara yake kuu ya mgahawa imeendelea kufanikiwa.
Kwa mujibu wa meneja wake, Gadner G Habash ambaye pia ni mumewe pamoja na kuwa na biashara yake ya Nyumbani Lounge, Lady Jaydee anatarajia kuongeza zaidi miradi mingine. “Huyu bado ni mjasiriamali mchanga anayejifunza zaidi na angependa kufanya biashara nyingi lakini muda ni mdogo. Isipokuwa kwa mwaka huu alitarajia kufanya kitu kingine kuongeza kama biashara. Hajawa tayari kusema ni kitu gani lakini mwenyezi Mungu akijaalia heri na afya mwaka huu kuna biashara nyingine Jaydee ataitambulisha, ukiacha Nyumbani Lounge na muziki,” Gadner aliiambia Bongo5 kwenye mahojiano maalum.
Mwaka huu Jide alipata pia endorsement kutoka kwenye kampuni ya vipodozi ya Sweden Oriflame Cosmetics na kuungana na wanawake wengine watatu maarufu wa Afrika Mashariki kuwa mabalozi wa bidhaa zao katika nchi zao. “Lady Jaydee, Juliana and Jamila have been named because their style and approach to beauty is the ideal representation for the Oriflame brand. They are strong and talented women who many people across East Africa readily identify with,”alisema mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Afrika Mashariki Mr. Klas Kronaas wakati akiwatangaza.
June 28, Lady Jaydee alikuwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza kwenye tukio la Masaku Rugby 7s After Party lililofanyika huko Machakos Kenya. Takriban watu 40,000 walihudhuria kwenye show hiyo iliyodhaminiwa na Tusker Lager. Wasanii wengine walitumbuiza ni pamoja na Jua Cali, Radio n Weasel, Wyre, Kidum, Keni wa Maria.
Kingine ni kubwa ni kuwa Lady Jaydee ataungana na Ali Kiba kutoka Tanzania kupanda jukwaa moja na Nicki Minaj, J Cole na wasanii wengine wa Marekani na Afrika kwenye tamasha la TribeOne Dinokeng litakalofanyika September mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Kingine ni kubwa ni kuwa Lady Jaydee ataungana na Ali Kiba kutoka Tanzania kupanda jukwaa moja na Nicki Minaj, J Cole na wasanii wengine wa Marekani na Afrika kwenye tamasha la TribeOne Dinokeng litakalofanyika September mwaka huu nchini Afrika Kusini.
AY
Kimuziki mwaka 2014, AY ameendelea kufanya movements nyingi ikiwa ni pamoja na kuachia wimbo wake ‘Asante’. Akiwa amebobea zaidi katika shughuli za ujasiriamali, mwaka 2014 umekuwa mzuri kibiashara kwake kutokana na kupata endorsement kuwa ikiwemo ile ya kampuni ya Samsung. Pia aliungana na Diamond kwenye mradi wa ‘Do Agric’ wa One Campaign.
Hivi karibuni pia, AY ambaye jina lake halisi ni Ambwene Yessaya pamoja na aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Faraja Kotta Nyalandu, waliteuliwa kuwa mabalozi wa UNICEF Tanzania katika mradi wa kupiga vita ukatili kwa watoto.
Akiwa mmoja wa waanzilishi wa kipindi cha TV kilichoshinda tuzo za watu, Mkasi, AY ana mpango wa kukivukisha boda.
Kwa mujibu wa mtandao wa Nairobi Wire, mwaka huu AY alienda Kenya na crew ya Mkasi inayomjumuisha mtangazaji Salama Jabir na Josh Murunga, kwa ajili ya kuangalia fursa zinazoweza kupatikana nchini humo kwa lengo la kutaka kupanua wigo wa kipindi hicho. “Tuko hapa kwanza kuangalia uwezekano wa kupanua biashara ya kipindi chetu” alisema AY.
Kwa mujibu wa mtandao wa Nairobi Wire, mwaka huu AY alienda Kenya na crew ya Mkasi inayomjumuisha mtangazaji Salama Jabir na Josh Murunga, kwa ajili ya kuangalia fursa zinazoweza kupatikana nchini humo kwa lengo la kutaka kupanua wigo wa kipindi hicho. “Tuko hapa kwanza kuangalia uwezekano wa kupanua biashara ya kipindi chetu” alisema AY.
Hata hivyo, kuna mambo mengi makubwa yanayoendelea katika himaya ya rapper huyo ambayo bado hajayaweka hadharani.
Nay wa Mitego
Nay wa Mitego ni rapper anayeendelea kuwashangaza wengi kwa mafanikio yake makubwa kimuziki na maisha yake binafsi. Rapper huyo ameendelea kuwa miongoni mwa rappers wa Tanzania wenye mashabiki wengi nchini huku nyimbo zake zikiwa na ushawishi mkubwa. Hivi karibuni, aliungana na Vanessa Mdee na Barnaba kama mabalozi wa kampeni ya Switch On ya Airtel.
Aliwashangaza watu wengi zaidi baada ya kuonesha nyumba yake ya kifahari aliyoijenga kwa takriban shilingi milioni 150 huku pia akimiliki magari ya bei.
“Gari yangu mpya Nissan Murano nimenunua milioni 36, ni gari ambayo naipenda sana ,dream car yangu kwenye maisha yangu ni Murano , ninaweza nikabadilisha nikawa na gari nyingine, pia mimi napenda nyumba nzuri ,napenda kuishi kwenye nyumba nzuri, nina nyumba tatu, hii hapa ambayo nahamia kesho ina thamani ya shilingi milioni 170 kila kitu, lakini inaweza ikawa zaidi ya milioni 170 kwasababu kuna vitu vingine huwa sivipigii hesabu,” Nay aliiambia Bongo5.
Vanessa Mdee
Vanessa Mdee aliwahi kuiambia Bongo5 kuwa mafanikio aliyoyapata sasa hakuwahi kuyafikiria. “Nilikuwa natarajiwa makubwa lakini haya ni makubwa haswaa. Ukiwa unafanya kazi ya muziki you hope for things to work out, you hope for things to be beneficial. Kwahiyo naona kama taratibu muziki wa Tanzania umebadilika na wasanii wameanza kupewa kipaumbele so I am just happy to do what I love to do,” alisema.
Mafanikio hayo ni pamoja na kushinda tuzo ya KTMA, kushiriki kwenye tour, kufanya matangazo ya biashara, kuchaguliwa kushiriki msimu wa pili wa Coke Studio Africa, kuhusishwa kwenye kipindi cha Introducing cha Channel O na mengine. Pamoja na kuwepo watu waliokuwa na mashaka na kipaji chake, Vee Money ameendelea kuwashangaza wengi na kujikusanyia mashabiki wa kila aina.
“Mpaka leo wapo wenye mashaka na mimi. Hainikatishi tamaa bali inanipa changamoto kuendelea kuwaprove wrong na kuendelea kufanya kitu kizuri mpaka wale waliokuwa na mashaka na mimi wakubali waseme ‘yeah she is the one’. So I don’t mind a few doubters,” anasema.
Ommy Dimpoz
Mwaka huu, Ommy Dimpoz ni miongoni mwa wasanii waliofanya show nyingi za nje kwa ziara ya Ulaya, Marekani na Asia. Pia amekuwa amekifanya show nyingi za nyumbani zinazomuingizia fedha nyingi. Diamond, amewahi kumtaja Ommy kama msanii anayefuata nyayo za mafanikio yake. Hili limedhihirika baada ya kuachia video ya wimbo wake ‘Ndagushima’ iliyoongozwa na Moe Musa.
Ommy Dimpoz aliiambia Bongo5 kuwa amepata jibu la kwanini kuwekeza na kufanya video nzuri kuna faida kubwa. Alisema hakutegemea kuwa kuna siku video yake itakuwa ikichezwa kama kawaida kwenye vituo vikubwa vya TV barani Afrika.”Kupigwa video kwenye channel kubwa sio tatizo, video nyingi sasa hivi zinaenda lakini unawashawishi vipi wakupe pia rotation? Ni Uzuri wa video, pengine wanaangalia director amefanya nani,” alisema.
Mwaka 2014, Ommy ameandaa show nyingi zake mwenyewe bila kutegemea promoter na hivyo kuingiza fedha nyingi zaidi na pia kumsaidia kuwa miongoni mwa wasanii wanaochaji fedha nyingi kutumbuiza.
Mwana FA
Hamis Mwinjuma aka Mwana FA ni msanii anayeongoza kwa kuyafanya mashairi ya nyimbo zake kugeuka sentensi kwenye midomo ya watu wengi. Mwaka huu wimbo wake ‘Mfalme’ umeongelewa zaidi mitandaoni na kuupa heshima ya hit isiyohitaji maswali.
FA ameendelea kuwa mchawi wa steji na mara nyingi yeye na AY wameendelea kuwa miongoni mwa rappers wakali jukwaani. Shughuli nyingi binafsi anazofanya Mwana FA zimeendelea chini ya kapeti lakini kuna mambo makubwa anayoyafanya.
Profesa J
Mwaka 2014, Mchawi wa Rhymes, Profesa Jay amerejea tena kwenye chart kwa ngoma yake ‘Kipi Sijaskia’ aliyomshirikisha, Diamond. Profesa ameendelea kujiimarisha kwenye miradi mbalimbali ya biashara ikiwa ni pamoja na kufungua studio yake ‘Mwanalizombe Recs’.
Pamoja na muziki, mwaka huu Profesa aliteuliwa kuwa mmoja wa mabalozi wa taasisi ya kilimo isiyo ya kiserikali (Ansaf) ambao hivi karibuni akiwa na AY walimkabidhi Rais Kikwete taarifa ya maoni kutoka kwa wakulima wa Tanzania, katika mkutano wa maswala ya kilimo uliyofanyika ndani ya hotel ya Double Tree.
Joh Makini & Nick wa Pili
Kwa mwaka 2014, Joh na mdogo wake Nick wamekuwa wakifanya mambo mengi ya muziki pamoja. Mwaka huu Weusi wamekuwa rappers wa Tanzania wenye video kali zaidi kuliko wote na zilizofika mbali. Walianza na ile iliyoongozwa na mshindi wa tuzo za watu, Nisher ya wimbo wao ‘Nje ya Box’ iliyoandika historia kwa kuwa video yao ya kwanza kuchezwa Channel O. Hawakusubiri kwa muda mrefu kwa kuachia video nyingine waliyoshoot Kenya ya ngoma yao ‘Gere’.
Pamoja na ngoma za Weusi, ndugu hawa wameendelea kushambulia kwa ngoma zao binafsi ambapo Nick aliachia wimbo ‘Staki Kazi’ uliopata shavu bungeni. Naye Joh Makini hivi karibuni aliachia single yake ‘Najiona Mimi’ aka I See Me’ iliyoendelea kumthibitisha kuwa mchawi wa hip hop. Weusi wameendelea kujimaarisha katika biashara zao kwa kuingiza sokoni bidhaa mbalimbali zikiwemo masweta, kofia, miwani na bidhaa zingine.
Fid Q
Fareed Kubanda aka Fid Q ameendelea kuwa rapper mwenye ushawishi mkubwa si tu kwa mashabiki wa hip hop, bali pia rappers wenzie. Uwezo wake wa kufikiri, maarifa anayoyapata kutokana na desturi yake ya usomaji wa vitabu, vimemfanya aendelee kuwa rapper mwenye mashairi makali zaidi Tanzania.
Pamoja na muziki, Fid ameendelea kujihusisha na shughuli za kijamii ikiwa pamoja na kusimamia vijana wa Hip Hop Darasa na pia kujihusisha na utengenezaji wa filamu za makala kuhusu masuala ya kijamii. Moja ya filamu aliyoshiriki kwa kusimulia ilioneshwa kwenye tamasha la ZIFF 2014 lililomalizika hivi karibuni.
Feza Kessy
Feza Kessy ana bahati ya kuwa msanii wa Tanzania mwenye mashabiki waaminifu nje ya nchi anayotokea. Uhusiano wake na mshiriki wa Big Brother Africa 2013, Oneal wa Botswana, umemfanya atengeneze kundi la mashabiki lijiitalo ‘Ninjas’ ambalo lipo nyuma yake katika shida na raha. Akiwa masomoni nchini Afrika Kusini, Feza ameendelea kufuata ndoto yake ya kuwa mwanamuziki mkubwa Afrika.
“Kunakuwa kuna shule, halafu kunakuwa na appearance job nafanya, just to appear as Feza Kessy , kuchukua picha na mashabiki na vitu kama hivyo. Pia sometimes nakuwa nafanya shows lakini sanasana inakuwa ni Botswana,” aliiambia Bongo5. Hivi karibuni, alishoot video ya wimbo wake mpya ‘My Papa’ na inatarajiwa kutoka hivi karibuni
0 comments:
Post a Comment