Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa chama cha kisiasa cha DP Christopher Mtikilaamefariki dunia alfajiri ya leo wakati akitokea Morogoro kuelekea Dar es salaam.
Taarifa zilizotufikia kupitia kwa kamanda wa Polisi Pwani Jafari Mohamed amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na alifarika saa 12 kasorobo katika kijiji cha Msolwa, Chalinze akiwa kwenye gari ndogo huku wenzake watatu wakijeruhiwa vibaya.
Mtikila alitangaza kugombea Urais kupitia chama chake cha DP lakini chama chake ni moja ya vyama ambavyo vilikatwa na NEC kutokana na kutotimiza baadhi ya masharti na vigezo vilivyomo kwenye fomu ya Mgombea Urai
s
s
#HabarizahiviPunde: Mwenyekiti wa Chama Cha DP Mch.Christopher Mtikila amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa katika ajali.
— ITV (@ITVTANZANIA) October 4, 2015
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na
Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata
habari mpya.
0 comments:
Post a Comment