Wananchi mkoani Arusha wametakiwa kuwa makini hasa katika kipindi cha uchaguzi na kuhakikisha kuwa wanapiga kura na kurudi mjumbani badala ya kubaki katika vituo vya kupiga kura kwani jukumu la usalama wa kura liko mikononi mwa vyombo vya usalama.
Hayo yameelezwa na mratibu wa Tume ya Uchaguzi mkoani Arusha ,Richard Kwitega akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Arusha, amesema kuwa kwasasa watatangaza utaratibu maalumu wa mawakala wa vyama vya siasa na wasimamizi wa tume pamoja na vyombo vya usalama kufanya kazi kwa pamoja na kuhakikisha matokeo yanabandikwa kila kata kuanzia ngazi ya udiwani,ubunge na urais.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amewataka wakazi wa Arusha kuondoa hofu wasiwasi juu ya uchaguzi kwa kuwa mamlaka zimejipanga kuimarisha hali ya ulinzi na usalama ili uchaguzi ufanyike katika mazingira mazuri…
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amewaasa wanasiasa kufanya kampeni za kistaarabu na kuepuka kuonesha alama za vyama vyao kwenye vyama vingine hali ambayo inaweza kusababisha vurugu.
Kampeni za uchaguzi zinaendelea kila kona ya Tanzania na zinatarajiwa kuhitimishwa na uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 ambapo watanzania watafanya maamuzi ya kuchagua viongozi kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge na urais.
0 comments:
Post a Comment