Headlines zilizochukua nafasi kubwa sana usiku wa September 24, 2015 taarifa ya Majonzi iliyosambaa na kuwafikia watu kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari pamoja na mitandao ya Kijamii, Serikali ikathibitisha pia kuhusu msiba wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mama Celina Kombani amefariki Dunia kutokana na maradhi ya Saratani.
Sasa jana Sept 25 jana nlipata taarifa kutoka nyumbani kwa marehemu akakutana na Michael ambae ni ndugu wa karibu wa marehemu na kazungumza naye..‘Kwa kweli mgonjwa baada ya kura za maoni alirudi nyumbani Dar akasema amechoka tukajua kwamba ni malaria tukampeleka hospitali ya TMJ akapata vipimo ikasemakana kwamba ni malaria huku akiendelea na matibabu mpaka siku ya mwisho alipoelekea India kufanya check up tu kama mtu wa kawaida ili arudi hapa aendelee na kampeni’ Michael
‘Ratiba ya mazishi bado haijakuwa sahihi lakini tunategemea kesho saa tisa na nusu mchana kuupokea mwili wa marehemu katika viwanja vya Airport Julius Nyerere ukitokea India, nakumbuka mara mwisho alikuwa ni mtu mwenye afya nzuri na wala hakuna mtu ambaye alitegemea katika leo litatokea hili, ameacha watoto watano (wakiume wane na wakike mmoja)’ Michae
l
l
0 comments:
Post a Comment