
Usiku wa December 7 2016 michuano ya UEFA Champions League hatua ya makundi ndio ilikamilika rasmi na timu 16 zilizofuzu hatua ya 16 bora zimefahamika, Real Madrid wao wamekamilisha hatua ya makundi kwa kucheza dhidi ya Borussia Dortmund.
Real Madrid wakiwa nyumbani katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu wenye uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya 80000 wamelazimishwa sare ya kufungana goli 2-2, Real Madrid ndio walikuwa wa kwanza kupata magoli mawili kupitia kwa Karim Benzema aliyefunga dakika ya 28 na 53.

Matokeo ya mechi za UEFA Champions League zilizochezwa usiku wa December 7 2016.
Dortmund wakiwa ugenini dakika 7 baada ya kufungwa goli la pili, Pierre-Emerick Aubameyang akapachika goli la kwanza kabla ya dakika ya 88 Marco Reuskuisawazishia Dortmund, mchezo huo pia umemalizika kwa Benzema kuwa mchezaji wa 6 kufikisha jumla ya magoli 5 katika michuano ya UEFA Champions League.

Wachezaji wanaoongoza kwa kufunga magoli mengi katika michuano ya UEFA Champions League

Timu zilizofuzu kucheza hatua ya 16 bora ya UEFA Champions Leagu
e
e
0 comments:
Post a Comment