www.kenethngamoga.blogspot.com

Mamilioni ya wafanyakazi duniani hatarini kupoteza kazi

March 25, 2017 imeripotiwa taarifa ya utafiti inayodai kuwa kuwa mamilioni ya wafanyakazi duniani wapo hatarini kupoteza kazi zao kutokana na matumizi ya Sayansi na Teknolojia.

Katika utafiti huo mpya uliofanywa hivi karibuni unaonesha kuwa kazi nyingi zitakuwa zinafanywa na robots miaka 15 ijayo ambapo Marekani ikiongoza kwa
38% ya kazi nchini humo zitafanywa na robots, kwa mujibu wa utafiti mpya wa PwC.
Wakati huo huo, 30% ya kazi Uingereza zitafanywa na robots, Ujerumani ni 35% huku Japan ikiwa 21% ya kazi ambazo zitafanywa na robots katika miaka 2030.
PwC imezitaja pia sekta zitakazoondoa watu wengi zaidi kwenye kazi na kutumia robots kuwa ni Usafirishaji, Viwanda, Maduka makubwa ya Jumla na Rejareja na sehemu ndogo katika Elimu, Afya na kazi za jamii. Wafanyakazi wa kiume wametajwa kuwa hatarini zaidi kupoteza kazi kuliko wanawake.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment