Mchezaji wa Azam FC ambaye amekuwa akiripotiwa kwa zaidi ya miezi kadhaa kuwa ataenda kujiunga katika timu ya Tenerife ya Hispania inayoshiriki Ligi daraja la pili Farid Musa huku akiwa amekwama Tanzania kwa madai ya vibali, leo December 27 2016 imetoka good news kuhusu dili hilo.
Azam FC kupitia kwa mkuu wao wa idara ya habari na mawasiliano Jafar Iddi amethibitisha kuwa timu ya Tenerife ya Hispania imekamilisha taratibu za tiketi na tayari imetuma tiketi ya ndege ambapo inaonesha kuwa Farid ataondoka kesho December 28.
Farid ataondoka Dar es Salaam kesho December 28 saa 23:00 akipitia Amsterdam, Barcelona na baada ya hapo ndio ataelekea Tenerife moja kwa moja, Farid alikwenda Hispania April 22 2016 kufanya majaribio na kufuzu ila alikwama kwa kuchelewa kupata kibali cha kazi.
0 comments:
Post a Comment