Ni siku moja imepita toka timu ya KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta, itangaze kuachana na kocha wake mkuu Peter Maes kutokana na mfululizo wa matukio yasiyoridhisha katika michezo ya hivi karibuni.
KRC Genk baada ya kuachana na Peter Maes leo imemtangaza kocha mpya atayerithi nafasi ya Peter Maes, Genk imetangaza Albert Stuivenberg aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Man United chini ya Louis Van Gaal.
Kama humfahamu vizuri Albert Stuivenberg aliwahi kuifundisha timu za taifa za vijana za Uholanzi kuanzia mwaka 2006 hadi 2013 alikuwa akiifundisha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 na baadae 2013/2014 kuifundisha timu ya vijana ya chini ya umri wa miaka 21
0 comments:
Post a Comment