Headlines za ajali ya ndege iliyokuwa imebeba msafara watu 72 wa timu ya Chapecoense ya Brazil na wahudumu 9 kuelekea Colombia kucheza mchezo wa kwanza wa fainali ya Sudamericana dhidi ya Atletico Nacional ya Colombia kupata ajali ndio habari ambayo inaripotiwa kwa kiasi kikubwa.
Moja kati ya wachezaji wachache wa Chapecoense waliosalimika kuwepo katika ajali hiyo ni kipa wa zamani wa Sporting CP ya Ureno Marcelo Boeck ambaye amejiunga na Chapecoense mwaka huu akitokea Sporting.
Wakala wa nyota huyo amesema golikipa huyo angekuwa sehemu ya msafara wa watu 72 wa timu waliokuwa katika safari hiyo, sema mchezaji huyo alikuwa kapewa ruhusa maalum ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa November 28 2016
.
.
0 comments:
Post a Comment