Moja kati ya habari au matukio makubwa yaliyotokea asubuhi ya November 29 2016 ni taarifa ya kikosi cha timu ya soka ya Chapecoense ya Brazil kupata ajali ya ndege wakiwa angani kuelekea kutua katika uwanja wa ndege wa Medellin.
Ndege hiyo kabla ya kuanguka katika milima ya Colombia ilianza kupotea katika rada, ndege hiyo ya shirika la ndege la Airline LaMia imethibika kuwa ilikuwa imebeba abiria 72 na wafanyakazi 9 wa ndege, abiria hao 72 wanaripotiwa wote walikuwa ni msafara na wachezaji wa timu ya Chapecoense ya Brazil.
Kikosi cha timu hiyo kilikuwa kinasafiri kuelekea Colombia kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa fainali ya Sudamerican dhidi ya Atletico Nacional ya Colombia ambapo mchezo huo ungechezwa Jumatano ya November 30 2016, kati ya watu 81 waliokuwemo katika ndege hiyo ni watu 5 ndio wametoka salama na 76 wameripotiwa kupoteza maisha.
0 comments:
Post a Comment