Usiku wa November 29 2016 timu ya Liverpool ilicheza mchezo wa EFL Cup dhidi ya timu ya Leeds United katika uwanja wa Anfield, katika mchezo huo Liverpoolwaliocheza katika uwanja wao wa nyumbani wamefanikiwa kushinda goli 2-0.
Magoli ya Liverpool yakifungwa na Divock Origi dakika ya 77 na Ben Woodburn dakika ya 81 kinda aliyefunga na kuvunja rekodi ya Michael Owen iliyodumu kwa muda wa miaka 19 toka Michael Owen alipoifungia goli Liverpool akiwa na umri wa miaka 17 na siku 145.
Ben Woodburn amekuwa ndio mchezaji wa Liverpool mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya Liverpool kuwahi kuifungia goli, goli hilo alilofunga dakika ya 81 amefunga akiwa na umri wa miaka 17 na siku 45 na kuvunja rekodi ya Michael Owen.
0 comments:
Post a Comment