www.kenethngamoga.blogspot.com

Samatta ameifungia magoli mawili KRC Genk dhidi ya Waasland-Beveren

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta usiku wa November 30 2016 ameingia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kuiongoza timu yake ya Genk kupata ushindi dhidi ya Waasland-Beveren


Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta usiku wa November 30 2016 ameingia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kuiongoza timu yake ya Genk kupata ushindi dhidi ya Waasland-Beveren.
Samatta akiwa na KRC Genk katika uwanja wa ugenini amefanikiwa kufunga magoli mawili katika ushindi wa goli 3-1, Samatta alifunga goli la kwanza dakika ya 15 goli la pili dakika ya 42 kabla ya mnigeria Wilfred Ndindi kufunga goli la tatu dakika ya 80.
Wenyeji wa mchezo huo Waasland-Beveren walifanikiwa kupata goli la kufutia machozi dakika ya 89, kupitia kwa mchezaji wao Zinho Gano, huo ulikuwa ni mchezo wa Kombe la Croky.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment