Wanasayansi
wanasema huenda ikawezesha binadamu kukabiliana na virusi hivyo iwapo
itafanikiwa, shirika la habari la AP linasema.
Wakati
wa majaribio hayo, ambayo yamepewa jina HVTN
702, wanasayansi wanatarajiwa kuwatumia wanaume na wanawake 5,400
ambao wanashiriki ngono kutoka maeneo 15 nchini Afrika Kusini.
Washiriki
hao watakuwa wa umri wa kati ya miaka 18 na 35.
Majaribio
hayo yatakuwa makubwa zaidi na ya kina zaidi ya chanjo ya Ukimwi kuwahi
kufanyika nchini Afrika Kusini ambapo zaidi ya watu
“Ikitumiwa
pamoja na silaha tulizo nazo sasa za kuzuia maambukizi, chanjo hiyo inaweza
kuwa msumari wa mwisho katika jeneza la Ukimwi,”
Anthony
Fauci, mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Maradhi ya Kuambukizana na Mzio ya
Marekani (NIAID) amesema kupitia taarifa.
“Hata
kama mafanikio yake yatakuwa ya kadiri, hilo linaweza kupunguza pakubwa mzigo
unaotokana na maradhi hayo katika nchi zenye viwango vya juu vya maambukizi,
mfano Afrika Kusini.”
Chanjo
ambayo itafanyiwa majaribio chini ya HVTN 702 ina uhusiano na majaribio ya
chanjo yaliyofanywa mwaka 2009 nchini Thailand.
Chanjo
iliyofanyiwa majaribio mwaka huo iligunduliwa kuwa na mafanikio asilimia 31.2
katika kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika kipindi cha ufuatilizi cha
miaka 3.5 baada ya mtu kupewa chanjo.
Wanasayansi
wametayarisha chanjo hiyo mpya mahsusi kutoa kinga pana na kwa muda mrefu na
kwa kuangazia zaidi aina ya virusi vinavyopatikana kusini mwa Afrika.
Watakaoshiriki
katika majaribio hayo ni watu wa kujitolea.
Wanachaguliwa
bila kufuata mpangilio wowote, ambapo kundi moja litapokea dozi ya chanjo kwa
kipindi fulani na jingine kipimo kisicho cha chanjo. Washiriki wote watadungwa
sindano tano katika kipindi cha mwaka mmoja.
Washiriki
watakaoambukizwa virusi vya Ukimwi katika kundi hilo watatumwa kwa wahudumu wa
afya ili kupokea matibabu ya kupunguza makali ya virusi hivyo na pia kushauria
jinsi ya kupunguza hatari ya kueneza virusi hivyo.
Afrika
Kusini ina zaidi ya watu 6.8 milioni ambao wanaishi na virusi vya Ukimwi.
Taifa
hilo hata hivyo limezindua mpango mkubwa wa kutoa dawa za kupunguza makali ya
ugonjwa huo na kuudhibiti, mpango ambao inasema ndio mkubwa zaidi wa aina yake
duniani.
Kiwango
cha wastani cha umri wa kuishi kilikuwa kimeshuka sana nchini humo na kufikia
miaka 57.1 mwaka 2009 lakini kutokanana na juhudi hizo, kimepanda hadi miaka
62.9 kufikia 2014.
Matokeo
ya majaribio hayo ya chanjo yanatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwaka 2020.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
0 comments:
Post a Comment