Kwa zaidi ya wiki sasa presha ya mchezo wa Ligi Kuu England kati ya Man United dhidi ya Liverpool ilikuwa ikitawala kwa mashabiki wa soka duniani kote, usiku wa October 17 katika dimba la Anfield ndio ilikuwa siku ya kumaliza ubishi wa mchezo huo, Liverpoolwaliwakaribisha Man United kucheza mchezo wao wa 193 katika historia.
Mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Man United ulikuwa unawakutanisha makocha ambao rekodi zao kwa mechi 5 zilizopita Jurgen Klopp amemfunga Jose Mourinho mara 3, sare moja na kapoteza mchezo mmoja, kitu ambacho kiliwafanya mashabiki wengi waamini kuwa Klopp anaweza akapata matokeo tena dhidi ya .
Liverpool walikuwa wanaweza kupata matokeo kutokana na kuwa nyumbani na rekodi ya kocha wao Jurgen Klopp dhidi ya Mourinho kuwa nzuri lakini waliambulia suluhu ya 0-0,Liverpool na Man United wanakuwa wametoka sare ya 45 katika michezo ya EPL na sare ya 52 kwa mechi za mashindano yote waliyowahi kukutana.
0 comments:
Post a Comment