www.kenethngamoga.blogspot.com

Joh Makini anachagua watu wakufanya nao kolabo,hivi ndivyo vigezo vyake..

Msanii wa hip hop kutoka kundi la Weusi Joh Makini amedai kuwa yeye huwa hafanyi kolabo tu na mtu yeyote bali huangalia mtu anayem feel.
Akiongea na SamMisago Joh ameweka wazi kuwa umaarufu wa mtu kwake sio kigezo cha yeye kufanya naye kolabo bali huwa anaangalia mtu ambaye anayeendana naye ili waweze kutengeza muziki mzuri na kuongeza kuwa watu wengi wanamlalamikia kuwa anapotezea makolabo.
Mimi niko very selective kwenye mambo ya kolabo..yani nachagua sana hata hapa bongo kuna malalamiko mpaka watu wengine wanakuuliza unataka shilingi ngapi,it’s not about the money,me naangalia mtu ambaye ninam feel,sio kwa sababu ana jina kubwa,nataka mtu ambaye tukiungana tunatoa muziki mzuri” alifunguka Joh Makini ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Perfect Combo.

Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment