www.kenethngamoga.blogspot.com

Kutoka TCRA wametoa ufanunuzi wa kufungiwa kwa simu feki….

Ni June 16, 2016 ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  yenye dhamana ya kusimamia shughuli za Mawasiliano ya Kielektroniki walizifungia simu feki zenye IMEI bandia44
Ni June 16, 2016 ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  yenye dhamana ya kusimamia shughuli za Mawasiliano ya Kielektroniki walizifungia simu feki zenye IMEI bandia
Sasa millardayo.com imepata meneja wa Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy na kueleza idadi ya IMEI zilizokamata na mtambo wao ambao umehusika kuzifungia simu feki.
‘Tukizungumzia ambavyo vimezimwa kinachofanyika kuzifunga zile IMEI bandia ambazo kwa jana tumefanikiwa kuzifunga simu zenye IMEI zipatazo laki sita na elfu 3 kwa maana ya kwamba unakuta simu moja ina IMEI mbili kwasababu simu yenye laini mbili ina IMEI mbili sasa ziko simu zenye IMEI hadi nne‘- Innocent Mungy
Kwahiyo ambacho tumeblock jana usiku ni IMEI laki sita ikiwa ina maana ni ambazo zinatumika kwenye simu feki, modem ya internet na IPAD, sasa sisi hatuwezi kutaja idadi ya simu ngapi tumezifungia ila tunachokijua ni kwamba IMEI laki sita ndio zimefungiwa zilizopo kwenye simu– Innocent Mungy
Zoezi hili bado linaendelea ambapo sasa hivi mtambo utakuwa unahakikisha simu zinazoingia bandia zitakuwa zinafungiwa, IMEI ni namba tambulishi  kama unakumbuka tulisema kwamba kila simu inayotengezwa inapewa namba tambulishi, sasa simu ili itengenezwe lazima ipite kwenye mchakato wa kuhakikisha kuna vitu ambavyo havitakiwi viwepo kwenye simu- Innocent Mung
y
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment