Siku moja baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya
Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kuweka wazi kuwa angependa Real Madri
dicheze na Benfica hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kauli hiyo aliitoa
kabla ya mchezo wa marudiano wa Benfica na FC Bayern Munich kuchezwa.
Siku moja baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kuweka wazi kuwa angependa Real Madridicheze na Benfica hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kauli hiyo aliitoa kabla ya mchezo wa marudiano wa Benfica na FC Bayern Munich kuchezwa.
Usiku wa April 13 2016 FC Bayern Munich ilicheza dhidi Benfica ya Ureno na kufanikiwa kuiondoa katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya goli 3-1, hivyo ndoto ya Ronaldo ya kutamani Real Madrid icheze na Benfica ikawa imeishia hapo.
Baada ya FC Bayern Munich kufuzu hatua ya nusu fainali kwa kuitoa Benfica, kocha waFC Bayern Pep Guardiola amemuomba Cristiano Ronaldo msamaha kwa kuikatisha ndoto yake ya kutamani Real Madrid icheza na Benfica nusu fainali, Guardiola aliongea katika lugha ya utani baada ya kuitoa Benfica.
“Samahani kwa kuivunja ndoto ya Ronaldo najua alipenda kucheza dhidi ya Benfica hatua inayofuata lakini haikuwezekana” >>> Guardiola
0 comments:
Post a Comment