www.kenethngamoga.blogspot.com

Majambazi Wauawa Dar, waliokuwa na mabomu pamoja na hirizi..

Taarifa iliyonifikia Leo March 21 2016 kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum Dar es salaam Simon Sirro ni hili tukio la majambazi watatu kuuawa katika eneo la Masaki mwisho Dar es salaam
Taarifa iliyonifikia Leo March 21 2016 kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum Dar es salaam Simon Sirro ni hili tukio la majambazi watatu kuuawa katika eneo la Masaki mwisho Dar es salaam.
Tukio lilikuwaje? Kamanda Sirro anasema ‘Mnamo tarehe 21 03 2016 majira ya saa 09:45, huko masaki mwisho watuhumiwa watatu wakiwa na gari namba T.125 BQJ RV4 Silver ,Bastola tatu na bomu la kurusha wakiwa kwenye harakati ya kumvamia mfanyabiashara mmoja aliyekuwa anapeleka fedha kwenye duka la kubadilishia fedha za kigeni
Askari walipata taarifa kutoka kwa raia wema, walifika haraka eneo latukio, ndipo wakakuta gari hiyo limepaki na kumwamuru jambazi aliyekuwa amebaki kwenye gari hilo afungue vioo na mtuhumiwa alikaidi amri hiyo na kufyatua risasi
Baada ya askari kuona hivyo wakaanza majibizano ya risasi na majambazi walifariki latika tukio hilo, baada ya kupekuliwa watuhumiwa hao walikutwa na Bastola tatu, bomu la kurushwa na mkono, nyundo moja, hirizi mbili, simu tatu na karatasi iliyoandikwa maneno ya Kiarabu
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment