www.kenethngamoga.blogspot.com

Mahujaji Watanzania waliofariki wafikia 25

Mahujaji wengine watatu kutoka Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tangu kutokea ajali ya kukanyagana kwa mahujaji Makkah nchini Saudia Arabia wametambuliwa ni miongoni mwa waliofariki dunia.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa jana jijini Dar es salaam imesema kutambuliwa kwa mahujaji kumefanya idadi ya mahujaji waliofariki hadi sasa kufikia 25.
Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa hadi sasa mahujaji 15 kutoka Tanzania bado hawajulikani walipo na jitihada za kuwatafuta zinaendelea huku wakisema miili ya mahujaji hao imeshazikwa nchini humo.
Majina ya mahujaji hao waliotambuliwa kufariki dunia ni Faiza Ahmed Omar na Rehema Ausi Rubaga kutoka kikundi cha Khidimat Islamiya na Masoud Juma Khamis kutoka kikundi cha Ahlu Dawaaa
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment