www.kenethngamoga.blogspot.com

Wananchi wasubiri kauli ya Magufuli kuhusu ajira, nyongeza ya mishahara

Mbeya.  Mamia wafanyakazi na wananchi wameendelea kumiminika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Edward Sokoine mkoani Mbeya, huku wakiwa na matarajio makubwa kutoka kwa Rais John Magufuli kuhusu ajira na nyongeza ya mshahara.
Wakizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatano Mei mosi 2019, baadhi ya wananchi wamesema wanatarajia Rais Magufuli atatangaza kuongezwa kwa mishahara ya wafanyakazi kwani kimekuwa ni kilio cha muda mrefu.
Sylvester Mwamboneke amesema anatarajia Rais Magufuli atatangaza kuongeza mshahara kwa wafanyakazi ikiwamo kutangaza kuongezwa kwa ajira.
"Wapo vijana wengi wa vyuo vikuu wamehitimu lakini hawajaajiriwa jambo ambalo limekuwa ni changamoto sana," amesema.
Naye Laison Tuyagaje amesema anatarajia kitu cha tofauti kutoka kwa Rais Magufuli kitakachokumbukwa kwenye historia ya wafanyakazi nchini.
Sherehe za kilele cha siku ya wafanyakazi zinafanyika mkoani Mbeya kitaifa, huku Rais Magufuli akiwa mgeni rasmi.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment