March 14 2017 moja kati ya stori zilizochukua headlines katika soka ni hii ya kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea Man United ya England Ander Herrera kuthibitika kufungiwa michezo miwili na chama cha soka cha England FA.
Herrera atakosa mechi mbili baada ya kuoneshwa kadi nyekundu ya pili ndani ya msimu mmoja, kadi ya kwanza alioneshwa dhidi ya Burnley October, Herrera sasa anaungana na Zlatan Ibrahimovic aliyefungiwa mechi 3 kwa kumpiga kiwiko Tyrone Mings AFC Bournemouth.
Kwa sasa ni rasmi Herrera atakosa mechi za Middlesbrough na West Brom lakini atakuwa na nafasi ya kuitumikia Man United katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA Europa League utakaochezwa alhamisi hii dhidi ya Rostov katika uwanja wa Old Trafford
0 comments:
Post a Comment