Msanii Nay wa Mitego ambaye anafahamika kwa kutoa ngoma zenye ukakasi kwa baadhi ya watu amekamatwa na polisi leo akiwa mkoani Morogoro alipokuwa amekwenda kufanya show.
Nay wa Mitego amethibitisha kukamatwa kwake baada ya kupost ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instgram
"Nimekamatwa kweli. Muda Huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza Kazi yangu iliyo ni leta. Napelekwa Mvomelo Police. Nawapenda Watanzania wote." aliandika Nay wa Mitego
Mpaka sasa bado haijafahamika sababu ya msanii huyo kukamatwa na polisi ingawa baadhi ya watu wanahusisha kukamatwa kwake kutokana na wimbo wake mpya unaofahamika kwa jina la 'Wapo' ambao umezungumzia mambo mengi ambayo yanatokea nchini kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment