www.kenethngamoga.blogspot.com

VIDEO: Jeraha lililopelekea Karelis wa KRC Genk kutakiwa kukaa nje miezi 8

Jumanne ya December 27 timu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta iliingia katika uwanja wake wa Luminus Arena kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya KAA Gent.
Mchezo huo ulimalizika kwa KRC Genk kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli yakifungwa na Pozuelo na Nikolaos Karelis ambaye aliumia dakika ya 48 kipindi cha pili na kushindwa kuendelea na mchezo na dakika ya 51 mtanzania Mbwana Samatta akachukua nafasi yake.
Taarifa zilizotoka leo December 28 2016 ni kuwa Karelis baada ya kufanyiwa uchunguzi jana na leo atafanyiwa upasuaji katika goti lake, upasuaji ambao utamfanya staa huyo kukaa nje ya uwanja katika kipindi cha miezi 8 hadi 9
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment