Genk wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani walianza kupata goli la uongozi dakika ya 3 kupitia Omar Colley kabla ya dakika ya 16 Orlando Carlos kufunga goli la kusawazisha na dakika ya 25 Ishak Belfodil kuongeza goli la pili na kuanza kuwa makini na ulinzi wa goli lao kuwadhibiti Genk.
Mchezo ulienda mapumziko KRC Genk wakiwa nyuma kwa goli 2-1 hali ambayo iliwawia vigumu kupata goli la kusawazisha mapema, Samatta ndio alikuwa mkombozi wa KRC Genk baada ya dakika ya 77 kupachika goli la kusawazisha kwa kichwa kupitia krosi iliyopigwa na Jere Uronen na kuufanya mchezo kumalizika kwa sare ya 2-2
0 comments:
Post a Comment