Moja kati ya habari zilizoingia kwenye headlines leo December 20 ni kuhusiana na statement iliyotolewa na Real Madrid kutoka mahakama ya michezo ya kimataifa CAS kuwapunguzia adhabu ya kutofanya usajili kwa kipindi chote cha mwaka 2017.
Statement ya Real Madrid inaeleza kuwa CAS wamewapumguzia adhabu iliyokuwa imetolewa na FIFA baada ya Real Madrid kukata rufaa kutokana na madai ya kukiuka kanuni za usajili kwa kumsajili mchezaji chini ya miaka 18 kinyume na taratibu.
Maamuzi ya CAS ni kuwa Real Madrid hawatafanya usajili katika dirisha dogo la mwezi January 2017 pekee na baada ya hapo wataruhusiwa, adhabu kama hiyo imewahi kuwakuta FC Barcelona lakini hawakupunguziwa, kitendo ambacho kinafanya wahoji kwanini wao walifanya usajili kwa kanuni kama walizozitumia Real Madrid na wametumikia adhabu ya mwaka mzima.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Real Madrid na Atletico walifungiwa na kamati ya nidhamu ya FIFA mwezi January kutofanya usajili kwa madirisha mawili kutokana na kukiuka kanuni za FIFA za usajili, kwa kufanya usajili wa wachezaji wa chini ya miaka 18 wasio raia wa Hispania, kosa ambalo limewahi kufanya na FC Barcelona na kutumikia adhabu yote.
0 comments:
Post a Comment