Moja kati ya stori zilizoingia kwenye headlines jioni ya November 26 ni kuhusiana na klabu ya Real Madrid ya Hispania kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya Sporting Gijon wakiwa wamevaa jezi zinazoangaza.
Jezi hizo ambazo zimetengenezwa na kampuni ya kijerumani ya Adidas, zimetengenezwa kwa kuyeyushwa plastiki laini iliyotokana na chupa zilizokuwa zimetupwa katika bahari ya Hindi, jezi moja inaripotiwa imetengenezwa kwa kutumia chupa 28.
Sababu ya kufanya hivyo Adidas wameshirikiana na Parley ambao ni wanaharakati na utunzaji wa mazingira kama sehemu ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa kuacha kuharibu vyanzo vya maji
.
.
0 comments:
Post a Comment