Baada ya headlines za muda mrefu zilizoanza toka October 10 2016 kuhusu hatma ya kocha mkuu wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans Hans van Pluijm kuwa anakaribia kufutwa kazi na nafasi yake kurithiwa na kocha wa Zesco United George Lwandamina.
Jioni ya October 24 2016 taarifa za kujiuzulu kocha huyo zimesambaa katika mitandao ya kijamii, huku wengi wakishangazwa na maamuzi ya kocha huyo kutangaza kujiuzulu,Hans amejiuzulu kufuatia kusikia ujio wa kocha wa Zesco United George Lwandaminaambaye inaaminika amekuja kuchukua nafasi yake.
Inadaiwa kuwa kilichosababisha viongozi wa Yanga kuwa katika mpango wa kumfuta kazi kocha Hans ni kutokana na kukataa kumrudisha kikosini Mrisho Ngassa aliyekuwa amevunja mkataba na Free State ya Afrika Kusini, Hans aliona hakuna haja ya kumrudisha Ngassa wakati kuna Deus Kaseke, Juma Mahadhi na Simon Msuva.
0 comments:
Post a Comment