Laudit Mavugo, (Kulia) akiwania mpra na beki wa Ruvu Shooting katika mechi ya leo la Ligi Kuu Tanzania Bara, uwanja wa Uhuru DSM
Katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Simba imefanikiwa kuichapa Ruvu Shooting mabao 2-1 katika mchezo mkali, na uliosheheni burudani ya aina yake licha ya kutawaliwa na kadi takriban 9 za manjano, na moja nyekundu.
Ruvu Shooting ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 9 ya mchezo kupitia kwa Mussa ambaye aliunganisha kwa shuti kali kutoka umbali wa takriban mita 18, mpira wa 'counter attack' baada ya Simba kukosa bao katika lango la Ruvu Shooting.
Simba iliyocheza soka la kushambulia zaidi, ilitulia na kufanikiwa kusawazisha bao kupitia kwa Ibrahim Ajibu aliyeunganisha kros ya Mohamed Hussein kutoka upande wa kushoto.
Simba ilipata bao la pili dakika ya 47 kupitia kwa Laudit Mavugo, aliyeunganisha vyema pasi ya Ibrahi Ajibu.
Hadi mwisho wa mchezo, Simba 2, Ruvu Shooting 1.
Katika mchezo huo Ruvu Shooting imemaliza ikiwa pungufu baada ya mchezaji wake Jabir Aziz kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi ya pili ya njano.
Mara baada ya mchezo huo, nahodha wa Simba, Jonas Mkude amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa kujitokeza kwa wingi na kuwataka waendelee kujitokeza uwanjani ili kuwaongezea ari ya ushindi.
Jijini Mbeya katika dimba la Sokoine, Azam FC imeendeleza moto wa ushindi baada ya kuichapa Prisons ya huko, bao 1-0, lililofungwa na Michael Kipre Bolou, dakika ya 59.
Mjini Mtwara katika dimba la Nangwana Sijaona, Yanga imebanwa mbavu na Ndanda FC, kwa kulazimishwa suluhu ya bila kufungana.
Simba na Azam zimefiksha pointi 7 katika michezo mitatu huku Yanga ikiwa na point 4 kwa mechi mbili ilizocheza hadi sasa. Ligi hiyo inaendelea mwishoni mwa wiki hii.
0 comments:
Post a Comment