September 6 2016 kampuni ya vifaa vya michezo ya kimarekani ambayo ina mkataba wa kibiashara na nahodha wa Man United Wayne Rooney wamemtengenezea kiatu nahodha huyo kwa ajili ya mchezo wa derby dhidi ya wapinzani wao wa mji mmoja Man City.
Hata hivyo mchezo wa Man United dhidi ya Man City utakaochezwa katika uwanja waOld Trafford, unatajwa kuwa na mvuto kutokana na kocha wa Man United Jose Mourinho na kocha wa Man City Pep Guardiola kuwa na uadui mkubwa na ndani ya uwanja toka wakiwa Hispania, hivyo watakuwa wanakutana tena kwa mara ya kwanza katika ardhi ya England.
0 comments:
Post a Comment