www.kenethngamoga.blogspot.com

Utafiti: Madaktari Afrika huzidisha dawa kwa wagonjwa

Utafiti unaonyesha kuwa madaktari wa nchi za kusini mwa Afrika wanatoa dawa nyingi zaidi ya zilizoagizwa na Shirika la Afya Duniani WHO
Inasemekana tatizo ni baya zaidi kwenye taasisi zinazotengeneza faida, na kuchochea kuuza dawa
Image captionInasemekana tatizo ni baya zaidi kwenye taasisi zinazotengeneza faida, na kuchochea kuuza dawa
Utafiti unaonyesha kuwa madaktari wa nchi za kusini mwa Afrika wanatoa dawa nyingi zaidi ya zilizoagizwa na Shirika la Afya Duniani WHO.
Utafiti huo uliofanywa na Chuo kikuu cha London kwa ushirikiano na kituo cha Kutoa ushauri wa afya cha nchini Ghana,ikihusisha nchi kumi na moja za kusini mwa jangwa la Sahara zinaonyesha kuwa wagonjwa wanapewa takribani dawa tatu kila wanapotembelea hospitali, moja zaidi ya maelekezo ya WHO.
Inasemekana tatizo ni baya zaidi kwenye taasisi zinazotengeneza faida, na kuchochea kuuza dawa.
Wagonjwa wengi wamekuwa wakipewa dawa za kutuliza maumivu pasipo kufanyiwa vipimo
Image captionWagonjwa wengi wamekuwa wakipewa dawa za kutuliza maumivu pasipo kufanyiwa vipimo
Tafiti zimeonya kuwa matumizi makubwa ya madawa yanasababishwa na kulazimishwa kutumia dawa, kuzidisha dozi na kuleta athari mbaya kwa mchanganyiko unaosababishwa na kuchanganya dawa mbalimbali.
Pia wamegundua wagonjwa wengi wamekuwa wakipewa dawa za kutuliza maumivu pasipo kufanyiwa vipimo, na kuongeza hatari ya maambukizo yanayosababisha na kupambana na dawa.
BBC
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment