Ni umbali mfupi kutoka katika mji Mkuu wa Ufilipino, Manila ambapo gereza la Quezon linapatikana likiwa halina miundombinu mizuri inayoshawishi jengo hilo kuitwa Gereza kwani sakafu ya jengo hilo ni takribani mita 30,000 za mraba, na wafungwa hutumia muda mwingi wakiwa wamesimama na wakijikunyata.
Gereza hilo lina takribani wafungwa 4000 na wengine wakizidi kuingia kila siku kutokana na vitendo vya uhalifu kukithiri katika mji wa Quezon wenye msongamano wa watu nchini Ufilipino.

160821115821-prison-cells-5-1-of-1-super-169Jengo la gereza la Quezon lilijengwa mnamo mwaka 1953,mamlaka inayohusika na gereza hilo imesema kuwa jengo hilo linafaa kupokea wafungwa 800 lakini viwango vya Umoja wa Mataifa vimesema kuwa gereza hilo linafaa kupokea wafungwa 200 tu.
“Chakula ni kibaya sana na pia ni ngumu sana kupata sehemu ya kulala hususani kipindi mvua zinanyesha”  anasema mfungwa mmoja katika gereza hilo (jina lake limehifadhiwa)
Hali ya ndani ya gereza hilo ni ya ajabu , hakuna sehemu inayoonekana ipo wazi , kila sehemu imesongwa na fulana za njano za wafungwa hao,asilimia 60% ya wafungwa katika gereza hili wamekutwa na hatia ya makosa  ya madawa ya kulevya.

160821115834-prison-cells-4-1-of-1-super-169
“siku zote gereza limekua likijaa lakini hivi karibuni idadi ya mahabusu imezidi mno” anasema mmoja wa askari magereza.
Wakosoaji nchini humo wanasema kujaa kwa gereza la Quezon ni matokeo ya athari za vita ya madawa ya kulevya ambayo Raisi Rodrigo Duterte ameianzisha tangu kuingia madarakani, na kama moja ya mambo aliyoahidi katika kampeni zake.



Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC)
a
Inmates peek from their cell inside the
d
Inmates sleep on the ground inside the Q
e