www.kenethngamoga.blogspot.com

Wanyama waliowahi kushinda nyadhifa uchaguzini

Mbwa kwa jina Duke amechaguliwa kwa mara ya tatu kuwa meya wa mji wa Cormorant jimbo la Minnesota, tunaangazia wanyama wengine ambao wamewahi kuchaguliwa kushikilia nyadhifa mbalimbali au kufanya kazi nyingine za binadamu.
Duke the DogImage copyrightFACEBOOK/DUKETHEDOGMAYOR

1. Mbwa waliowahi kuchaguliwa kuwa mameya

Kuna Junior Cochran, mbwa mweusi aina ya Labrador, aliyechaguliwa kuwa meya mji wa Rabbit Hash, Kentucky, mwaka 2004.
Na hatuwezi kumsahau Bosco mbwa aliyehudumu kama meya wa Sunol, California, kuanzia 1981 hadi 1994.
Hata kuna sanamu ya ukumbusho wake.
BoscoImage copyrightANDREW RICHARDSON
Image captionSanamu ya mbwa aliyejulikana kama Bosco

2, Paka waliochaguliwa kuwa mameya

Paka kwa jina Stubbs alichaguliwa meya wa Talkeetna, Alaska, mwaka 1997.
Kuna hata akaunti ya Twitter yenye jina lake. Kwenye maelezo imeandikwa: "Mimi ni paka. Nilichaguliwa Meya wa Alaska. Karibuni, nitakuwa rais."
StubbsImage copyrightJENNI KONRAD
Image captionPaka kwa jina Stubbs
3. Kifaru 'taka' aliyechaguliwa kuongoza Sao Paulo
Mwaka 1959, kifaru wa umri wa miaka mitano kwa jina Cacareco alichaguliwa meya wa mji wa Sao Paulo kwa kura nyingi sana.
Cacareco, jina ambalo maana yake ni "taka" kwa Kireno, aliandikishwa kwenye kura kama hatua ya kulalamikia ufisadi miongoni mwa wanasiasa.
Hakuchukua mamlaka hata hivyo kwani uchaguzi ulirudiwa.

4. Mbuzi kiongozi wa New Zealand

Iwapo bado umeshangaa, tulia. Eneo la Whangamomona nchini New Zealand, mbuzi kwa jina Billy Gumboot mwaka 1999 alichaguliwa kuwa rais.
Alikuwa mnyama wa kwanza kuchaguliwa katika wilaya hiyo lakini hakuwa wa mwisho, baada yake kuondoka madarakani, mrithi wake alikuwa mbwa aina ya Poodle aliyepewa jina Tai.
Kwa sasa eneo hilo linaongozwa na rais wa kwanza mwanamke, Vicki Pratt.
5. Sokwe wa Rio de Janeiro
Sokwe kwa jina Tiao alipata kura nyingi, ingawa hazikutosha kabisa kumfanya meya wa mji wa Rio de Janeiro. Kauli mbiu yake ilikuwa: "Mpigie kura tumbili - upate tumbili."
Lakini alipata sanamu.
TiĆ£oImage copyrightFULVIUSBSAS
Image captionSanamu ya Tiao
6. Penguini brigadia
Penguini kwa jina Nils Olav alipewa hata cheo cha Brigadia katika jeshi la Norway, na hata akakubaliwa kutekeleza majukumu rasmi, mfano kukagua gwaride.
7. Paka kiongozi wa chama cha kisiasa Uingereza
Paka kwa jina Mandu, kutoka Uingereza, alihudumu kama kiongozi mwenza wa chama cha Official Monster Raving Loony Party kuanzia 1999 hadi 2002.
Ndiye paka pekee aliyewahi kuongoza chama cha kisiasa.
Tovuti ya chama hicho inasema: "Kilikuwa kinyang'anyiro kikali kati ya Howling 'Laud' Hope na Paka Mandu.
"Walikaribiana sana kwa kura. Wote walipata kura 112 kila mmoja na ikaamuliwa washikilie wadhifa huo kwa pamoja."
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment