www.kenethngamoga.blogspot.com

YAMEMFIKA HAPAAA 🤔 | ZARI ATUMA UJUMBE MZITO KWA WAKWE ZAKE KUPITIA MTANDAO WA SNAPCHAT #USIPITWE

Diamond Platnumz na Zari the Bosslady wapo kwenye mtihani mgumu unaozikumba familia nyingi za Kiafrika – maelewano hafifu na ndugu wa ukweni! 






Diamond Platnumz na Zari the Bosslady wapo kwenye mtihani mgumu unaozikumba familia nyingi za Kiafrika – maelewano hafifu na ndugu wa ukweni! 
Mama Tiffah yupo mjini alipokuja kumsalimia mchumba wake huyo na kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mama mkwe wake.
Licha ya Diamond kupost kipande cha video controversial Instagram wakiwa bafuni na mpenzi wake – wengi wanasema uso wa Zari unaonesha sura tofauti, ya huzuni tofauti na anavyoonekana mwenzie. 

Kuna mengi yalitokea kwenye birthday ya Mama Diamond na ambayo yanazungumzwa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia urafiki usio wa kawaida wa dada yake Diamond, Esma na Hamisa Mobetto na mengine. Esma amelifafanua hilo kwa post ndefu Instagram.



Lakini kubwa ni ujumbe wa kutatanisha wa Zari kwenye mtandao wa Snapchat unaoelezea jinsi ambavyo hajali ukoo mzima usipomkubali.



“Hakuna mtu mwenye uhusiano na dunia nzima, nchi au ukoo,” aliandika kwenye Snapchat, mtandao ambao wasanii wanaamini wana uhuru wa kufunguka zaidi.

“Huwa na uhusiano na mwanaume au mwanamke wao, ni mimi na yangu tu ndivyo vyenye maana. Unataka kujua kwanini? Ni sababu ilikuwa ni nyie wawili tu pindi mlipokutana. Na itakuwa ninyi wawili tu pindi mambo yakienda kombo kati yenu. Haitakuwa ukoo au nchi au mtu mwingine wa tatu,” aliongeza.
Bi. Sandra ambaye ni mtumiaji mzuri wa Instagramm aliweka petroli kwenye moto baada ya kupost picha ya Wema na Idris na kuwasifia: Uzalendo kwanza, umependeza sanaa mamy akee..”


Binamu wa Diamond, Romy Jones naye amepost picha kumpongeza shemeji yake wa zamani. Wanasema ushemeji haufagi lakini.


Kuna mjadala mzito Instagram kuhusu issue hii. 


Tetesi za kuwa Zari hana maelewano mazuri na ndugu zake na Diamond zimekuwa zikiandikwa kwa muda mrefu na magazeti ya udaku. Kwa yaliyotokea, kuna asilimia nyingi za ukweli ndani yake.
Hakika Diamond kazi anayo!
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment