Mfanyabiashara maarufu aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa anajipatia milioni 7 kila dakika, Mohamed Yusufali amepandishwa tena kizimbani leo July 26 2016 mahakama ya Kisutu akiwa na mfanyabiashara maarufu wa Arusha na Dar es Salaam Samuel Lema wakibaliwa na mashtaka 222 likiwamo la ukwepaji kodi ya zaidi ya Sh bilioni 14.
Katika shtaka la pili la kughushi inadaiwa walilitenda Julai 17, mwaka jana jijini Dar es Salaam ambapo kwa pamoja walitengeneza hati ya uongo ili kuonyesha Kampuni ya Northern Engineering Works Limited imenunua hisa za kampuni ya Farmplant Dsm Limited kwa Sh.milioni 4.3 huku wakishindwa kulipa kodi na wakijua kuwa ni uongo.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Hakimu Mashauri aliwaambia washtakiwa hao kuwa hawatakiwi kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria ya kusikiliza kesi hiyo.
Hata hivyo, Hakimu Mashauri alikubaliana na hoja ya upande wa jamhuri na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 28 mwaka huu ambapo upande wa jamhuri utawasilisha majibu ya hoja zilizowasilisha na utetezi katika kesi hiyo huku washtakiwa hao wakirudishwa lumande
.
.
0 comments:
Post a Comment