Baada ya jana June 8 klabu ya Man United iliyopo chini ya Jose Mourinho kufanikiwa kufanya usajili wake wa kwanza kwa kunasa saini ya Eric Bailly kutoka Villerreal yaHispania, leo June 9 2016 wameripotiwa kutenga kiasi cha pound milioni 47 ambazo ni zaidi ya bilioni 140 za kitanzania kwa ajili ya kuishawishi Juventus ya Italia iwauzie Alvaro Morata.
Tofauti na ilivyokuwa inatarajiwa na wengi kuwa Zlatan Ibrahimovic ndio staa atakayefuatiwa kusajiliwa Man United baada ya Eric Bailly, lakini taarifa zimetoka kuwa Man United wanalazimika kuchelewesha usajili wa Zlatan hadi June 31 ili amalize mkataba wake rasmi na PSG, kwani akisaini wakati huu atalazimika kuilipa PSG kutokana na mkataba wake kuwa na kipengele cha uaminifu.
Hivyo Man United wanatajwa kuwa na mipango ya kumsajili Alvaro Morata ambaye atakuwa anafanya kazi kwa mara ya pili na Jose Mourinho, baada ya awali kuwahi kufanya nae kazi wakiwa katika klabu ya Real Madrid ya Hispania, Mourinho ndio kocha aliyeanza kumuamini Morata na kumpata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment