Mahakama ya Hakimu Mkazi Ilala jijini Dar es Salaam, imeiamuru kampuni ya
mawasiliano ya TIGO kuwalipa wasanii Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Ambwene
Yessayah ‘AY’ jumla ya shilingi bilioni 2.18 baada ya kutumia kazi zao za
muziki bila ridhaa yao.
Hukumu
hiyo imetolewa kutokana na kampuni hiyo kutumia kazi za wasanii hao ‘Dakika
Moja’ na ‘Usije Mjini’ kama miito ya simu bila makubaliano yoyote. Hiyo inakuwa
hukumu kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwenye historia ya mambo ya ukiukwaji wa
haki miliki za kazi za ubunifu na sanaa nchini.
Hakimu
mkazi wa mahakama ya Ilala, Juma Hassan alitoa hukumu hiyo Jumatano hii
kufuatia mvutano mahakamani kati ya pande hizo mbili uliodumu kwa kipindi cha
miaka minne. Pia Tigo imetakiwa kulipa shilingi milioni 25 nyingine kama sehemu
ya fidia.
Taarifa
za kesi hiyo zimefahamika wiki hii baada ya wakili wa mastaa hao Alberto Msando
kupost kwenye Instagram picha akiwa nao kwenye mahakama kuu jijini Dar es
Salaam.
“At
the High Court of Tanzania, Dar Es Salaam. #UsijeMjini #DakikaMoja #Tigo
#CopyrightsInfringement #stoppingwizi @aytanzania @mwanafa,” aliandika.
Kampuni
hiyo ilikuwa imepeleka pingamizi la hukumu hiyo ya mahamaka ya hakimu mkazi
Ilala katika mahakama kuu ya Tanzania. Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa Jumanne
hii lakini imeahirishwa hadi Ijumaa.
Madai
ya Mwana FA na AY ni kuwa Tigo ilitumia kazi zao bila kuwa na mkataba nao
wowote au kampuni ya kati iliyowawakilisha na hivyo kuingiza fedha ambayo
wawili hao wanaamini ni nyingi.
Awali
walitaka walipwe fidia ya shilingi bilioni 4.3.
Chanzo: The Citizen
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na
Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata
habari mpya.
0 comments:
Post a Comment